Rais wa Kenya William Ruto, ameitisha kikao cha dharura cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki mwezi ujao kujadili changamoto ya kifedha ambayo imetatiza shughuli za taasisi za jumuiya hiyo, tatizo kubwa likiwa baadhi ya nchi kuchelewesha kutoa michango kwa wakati.
Mkutano huo utajadili mfumo mpya wa uchangishaji fedha na namna ya kupunguza matumizi ya jumuiya hiyo.