Mwishoni mwa juma Afrika Kusini ilitangaza kuondoa wanajeshi wake kutoka kwa tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini DRC (MONUSCO) baada ya kikosi hicho kuhudumu kwa miaka 27.Pretoria inasema hatua hiyo ni kutokana na mipango yake ya kurekebisha na kuimarisha raslimali ya jeshi lake.Tumemuuliza msikilizaji anazungumziaje hatua hii ya Afrika kusini,Hatua hii ni kumaanisha Monusco imepoteza nguvu DRC na Nini kifanyike kuleta usalama wa kudumu nchini DRC?