Timu ya DRC "Leorpard" siku ya Jumanne ilikuwa mwakilishi wa mwisho wa Afrika Mashariki kuondolewa kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, baada ya kupoteza mechi yao ya hatua ya 16 bora dhidi ya Algeria. Uganda ilikuwa ya kwanza kuondolewa katika hatua ya makundi ikifuatiwa na Tanzania iliyotolewa kwenye hatua ya mtoano.