leo tunazungumzia kuhusu Hatua ya kukamatwa kwa mshauri wa mwanasiasa wa upinzani nchini DRC Moise Katumbi Salomon Idi Kalonda kumeibua mjadala kuhusu namna vyombo vya usalama na sheria vinatumika kisiasa kujaribu kuwanyamazisha wapinzani.
Kilochotokea nchini DRC kimeshuhudiwa Senegal, Guinea na hata Uganda wakati mmoja.
Unadhani ni njama za serikali zilizoko madarakani kubana wapinzani?Matukio kama haya yanashuhudiwa nchini mwako?