|
Nchi za Marekani na Saudia ambazo zimekuwa zikiratibu mazungumzo ya kuleta amani Sudan zimetaka mazungumzo hayo kufanyika upya . Leo hii ,tunajadiliana kuhusu wito wa Marekani na Saudi Arabia,mwishoni mwa wiki ,kutaka kufanyika upya kwa mazungumzo ya amani kati ya pande hasimu zinazopigana nchini Sudan wakati huu mapigano makali yakiendelea kushuduiwa. Hivi Unaamini kuwa nchi za kikanda zinashindwa kutatua tatizo la Sudan? Unafikiri ni wakati mwafaka wa kuwatuma askari wa kulinda amani nchini Sudan na Nini kingine kinaweza kufanyika ile kuleta suluhu la kudumu? |