|
Description:
|
|
Nchini DRC upinzani umelaani polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kuyazima maandamano yao mwishoni mwa juma lililopita jijini Kinshasa, wakati video ikionesha polisi wakimdhalilisha na kumpiga kijana moja ikiendelea kusambaa mitandaoni. Mwanasiasa mwengine wa Upinzani amejikuta msafara wake umezuiwa kuelekea katika eneo la Congo central hivi leo kuenda kukutana na wafuasi wake. Tumekuuliza msikilizaji unafikiri polisi wanastahili kuwa tabia gani? Je polisi nchini kwako hukabiliana na maandamano vipi? Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kupata maoni zaidi |